Habari Mpya

Friday, June 17, 2016

Zifahamu Dhambi Ambazo Huondolewa Na Papa Pekee Au Padre Kwa Mamlaka Maalumu Kutoka Kwa Papa :

Kanisa katoliki limekuwa na taratibu zake katika eneo la kutubu dhambi,  kwa Msaada wa mtandao wa wakatoliki nchini inakuletea mchanganuo wa dhambi ambazo huondolewana Papa na mamlaka yake.
1.Kumdhuru baba mtakatifu kimwili mfano:kumpiga au kumtemea mate
2.Kukufuru Ekaristi Takatifu mfano kutema na kuchezea kwa namna yoyote kama ya kishirikina.
3.Padri kutenda dhambi na muumini mfano : kuzini
4.Askofu kumpa padre uaskofu padre yeyote bila ruhusa ya baba mtakatifu.

NB:jiandae kufanya kitubio kama unaguswa na dhambi yoyote kati ya hizo kwani kuna mchakato maalumu wa kuteuliwa kwa mapadre zaidi ya 800 na baba mtakatifu kwenda dunia zima kwa kuwaondolea watu wenye dhambi hizo. Tumsifu Yesu Kristu
Kuhusu dhambi namba 3 inakosa tu maelezo.Na maelezo yake ni haya;

Padre kuzini na muumini hiyo inabaki kuwa ni dhambi Kati ya Padre na muumini wake.Kwa dhambi hiyo Padre anaweza akatafuta Padre mwenzake akaungama kadhalika na kwa muumini huyo.

Shida ni pale tu endapo,Padre anataka KUMUUNGAMISHA mwanamke (muumini) aliyetoka KUZINI naye au yule ANAYEZINI naye hiyo dhambi na kosa hilo hata Askofu wako hana mamlaka ya kukuungamisha wala kukusamehe ni kiti cha Baba Mtakatifu pekee chini ya Congregatio inayoshughulikia mambo matakatifu iitwayo kwa kifupi CDF yaani Congregation for Doctrine of Faith.

Ambayo inashughulikia na mambo mawili hasa makuu yaani;
1.Protection of Sanctity of Sacraments
2.Dealing with Grave Disorders and bad conducts in the Church.
Kwa ufupi ndio hivyo ninaweza kukwambia

Taarifa hii ni kwa msaada wa mtandaao wa wakristu wakatoliki nchini
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Zifahamu Dhambi Ambazo Huondolewa Na Papa Pekee Au Padre Kwa Mamlaka Maalumu Kutoka Kwa Papa : Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top