Habari Mpya

Friday, June 17, 2016

Wanamuziki Wakongwe nchini wanamengi ya kujifunza toka kwa Emmy Kosgei na Video yake mpya,

Emmy Kosgei Madubuko ni mwanamuziki mkongwe toka nchini Kenya ambaye kwa sasa anaishi na familia yake nchini Nigeria, hivi karibuni Emmy akiwa nchini Kenya ameachia nyimbo yake mpya iitwayo TAI.

Katika Video hiyo Emmy ameifanya katika ubora wa hali ya juu japokuwa kwa muonekanao tu haikutumia gharama kubwa sana ukilinganisha na ubora wa kazi iliyotoka .Ndani ya VIDEO hiyo  kuna Location kubwa mbili tu barabarani pamoja na ndani ambako kumechukua sehemu kubwa ya Video kwa kutumia Blue screen.

Rangi nzuri ya Video na umakini wa director Tiger toka Mind Vision Production  ndio hasa kumepelekea ubora wa video hii, somo ambalo wakongwe nchini wanapaswa kulipata hapa ni kwamba sio lazima kila video iwe na location lukuki mara kwenye maua,beach,Hotelini,kanisani,chini ya miti na kadhalika Noooo.

Emmy alichofanya kikubwa Kwanza ni kuchagua kufanya kazi na Kampuni Nzuri inayoeleweka, pili Kuamua kuonyesha utofauti wa video kwa kuja na video simple but Quality na haya yote kina Bukuku,Frola Mbasha,Jenipher Mgendi,Upendo Kilahilo(Upendo j Bridge),Bonny Mwaitege, na wengine wengi wanaweza.

Christina Shusho,na Miriam Lukindo ndio wanamuziki wakongwe nchini ambao kila kukicha wanazingatia ubora katika video zao, ukienda hatua nyingi mbele utagundua mafanikio ya wawili hawa ni kutokana na exposure waliyonayo pamoja na umakini wa watu wanaowazunguka.

Muda umefika kwa wakongwe nchini kubadilika na na kuufikisha muziki wa Injili mbali zaidi kupitia kazi zao.Kwa sasa Mwanamuziki unapotaka kufanya Muziki wa injili usiifikirie Mbeya,Arusha, Kagera na Kigoma Noo angalia nyimbo yako ikifika Zimbabwe,Nigeria, na afrika kwa ujumla kama sio dunia nzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Wanamuziki Wakongwe nchini wanamengi ya kujifunza toka kwa Emmy Kosgei na Video yake mpya, Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top