Habari Mpya

Saturday, July 02, 2016

Gospel Lyrics: Mwema By Mercy Masika

Mwema ni moja nkati ya nyimbo kutoka kwa mwanadada Mercy Masika wa nchini Kenya,Mercy Masika kwa sasa ndiye mwanamuziki Bora wa Kike nchini humo na hii ni kwa mujibu wa tuzo za Groove Awards 2016.

Nyimbo hii imejizolea umaarufu na kuwabariki wengi ndani na nje ya bara la Africa.Hapa chini Hosanna Kwanza inakuletea mistari iliyomo ndani ya nyimbo hiyo.

Wako mwana ukamtuma, duniani

Kisa na maana nipate uzima jamani

Ishara kwamba unanipenda zaidi

Hivyo nishaelewa sifa nitakupa zaidi


Chorous

Na siwezi jizuia, kusema wako wema

Na sio kama najigamba, umenitenda mema

(Repeat)

Umekuwa mwema kwangu

Umenitoa gizani, nilipokuwa nimeshikwa mateka

Ukanipa tumaini, kwako nikajificha

Sasa nitakupa nini, iwe sawa na yale umenitenda?

Hakuna ila moyoni, sifa nitakuimbia

Ilikugharimu, msalabani unifie

Hivyo inanibidi, sifa nikuimbie

Wema wako niseme, ili na wengine wakujue

Wote waungane nami, na wazee ishirini na nne

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Gospel Lyrics: Mwema By Mercy Masika Description: Rating: 5 Reviewed By: mcjohnminja.blogspot.com
Scroll to Top